Ujumbe wa SMS
Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: TUMA UJUMBE MFUPI: Idhaa ya Kiswahili ya Radio Deutsche Welle, sasa inajisogeza karibu na wasikilizaji na ili tuwe karibu nanyi, tunawakaribisha kushiriki katika matangazo yetu ya kila siku.
Kila siku tunawaletea uchambuzi wa ripoti za matukio ya kimataifa na yanayotokea Afrika, kutoka kwa waandishi wetu, pamoja na mahojiano na wanaohusika na matukio hayo.
Hakika kutoka hapa Ujerumani, Radio Deutsche Welle TUNAVUMA KWA KISHINDO.
Kwa hayo yote sasa tunakupa fursa ya kutuma maoni yako moja kwa moja wakati wa matangazo yetu ya mchana na jioni, juu ya ripoti utakazozisikia, kwa kutuma ujumbe mfupi ama SMS kupitia simu yako ya mkononi, Jumatatu hadi Ijumaa. Kumbuka ujumbe uhusike na ripoti tutakayoitangaza wakati huo.
Tuma ujumbe wako kwa nambari:
+ 49 17 32 91 17 90.







